# TANZANIA ASSOCIATION FOR PUBLIC ADMINISTRATION AND HUMAN RESOURC ## Posts - [Hello world!](https://tapahr.org/hello-world/): Welcome to WordPress. This is your first post. Edit or delete it, then start writing! - [WIZARA KUPIMWA KWA UTEKELEZAJI WA MWONGOZO WA UJUMUISHAJI WA JINSIA KATIKA UTUMISHI WA UMMA](https://tapahr.org/wizara-kupimwa-kwa-utekelezaji-wa-mwongozo-wa-ujumuishaji-wa-jinsia-katika-utumishi-wa-umma/): Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amezitaka Wizara zote kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mwongozo wa Ujumuishaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma kila mwisho wa mwaka katika Ofisi hiyo ili kuhakikisha Mwongozo huo unatekelezwa kwa ufanisi kama ilivyokusudiwa na Serikali. Bw. Daudi amezungumza hayo leo wakati akifunga semina elekezi ya siku mbili ya Mwongozo wa Ujumuishaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma kwa Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara pamoja na Waratibu wa Jinsia Ngazi ya Wizara iliyofanyika jijini Dodoma. Amesema kuwasilisha taarifa ya utekelezaji na kupimwa […] - [MHE. SANGU: UADILIFU NI MSINGI WA USALAMA WA TANZANIA](https://tapahr.org/mhe-sangu-uadilifu-ni-msingi-wa-usalama-wa-tanzania/): Tuwawajibishe au kuachana na watumishi wasiokuwa waadilifu kwa kuwa sisi ndio tunaotakiwa kusimamia uadilifu lakini miongoni mwetu tunakuwa na watu wasiokuwa waadilifu” Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu wakati akiongea na viongozi na watumishi wa TAKUKURU makao makuu Dodoma. Amewakumbusha Viongozi na watumishi hao kuwa suala la uadilifu limeandikwa hata katika vitabu vya dini zote ambapo likizingatiwa kwa usahihi amani na utulivu hutamalaki miongoni mwa wananchi. Alisema, TAKUKURU ni taasisi muhimu na nyeti katika taifa la Tanzania na msingi wake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano […] - [MHE. SIMBACHAWENE AWAASA WAHITIMU KUSHIKA ELIMU KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU.](https://tapahr.org/mhe-simbachawene-awaasa-wahitimu-kushika-elimu-kwa-ujenzi-wa-taifa-endelevu/): Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewaasa wahitimu wa darasa la Saba kushika elimu kwa kuwa elimu ni msingi wa maisha na inajenga taifa endelevu. Mhe. Simbachawene alisema kuwa, Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua umuhimu wa elimu kwa taifa, hivyo, amewekeza zaidi katika elimu ikiwa ni jitihada za kuendelea kupambana na maadui watatu wa Taifa ambao ni ujinga, umasikini na maradhi. Aidha, aliwakumbusha kuwa msomi ni mtu yeyote ambaye amefuta ujinga, anaweza kusoma na kuandika na kutanzua mambo yanayomkabili, hivyo elimu ni muhimu na ndiyo mana Serikali […] - [MHE. SIMBACHAWENE AMTEMBELEA MAMA SITTI MWINYI](https://tapahr.org/mhe-simbachawene-amtembelea-mama-sitti-mwinyi/): Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amemtembelea Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo Septemba 10, 2024. “Rais, amenielekeza kuwafikishia salaam zake na amesema yuko pamoja nanyi na ndio mana amenituma kufika hapa nyumbani na kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi” amesema Mhe. Simbachawene. Mhe. Simbachawene amesema Rais Mhe. Dkt. Samia anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria. Aidha, Mama Sitti amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kupata nafasi ya […] - [MHE. SIMBACHAWENE ATETA NA RAIS KIKWETE](https://tapahr.org/mhe-simbachawene-ateta-na-rais-kikwete/): Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete nyumbani kwake Kawe Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Simbachawene amefikisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameahidi kuendelea kuwa pamoja na Viongozi Wakuu Wastaafu wa Kitaifa kwa maendeleo ya taifa. Mhe. Simbachawene amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina jukumu la kutunza Viongozi Wakuu Wastaafu Kitaifa na Wenza […] - [NAIBU WAZIRI AWAFUNDA WANAJOPO WA KADA YA AFYA](https://tapahr.org/naibu-waziri-sangu-awafunda-wanajopo-wa-kada-ya-afya-asisitiza-uadilifu/): Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus  Sangu amewataka wanajopo la usaili kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wanatenda haki huku akisititiza  ajira  ni suala la usalama wa nchi. Ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha wakati akizungumza na wataalamu kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za Serikali ambao wamechaguliwa kuwa  wanajopo wa kuendesha zoezi la usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa  wasailiwa kada ya afya unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini. Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha  haki inatendeka  kwa kila msailiwa ili atakayeshinda ashinde kwa haki na atakayeshindwa ashindwe kwa haki. Mhe. Sangu ametumia fursa hiyo […] [comment]: # (Generated by Hostinger Tools Plugin)