ABOUT TAPA-HR
TAPA-HR ni Jumuiya ya Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala katika Utumishi wa Umma ambayo imeanzishwa chini ya Sheria ya Msajili wa Vyama Sura 337 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 na kupewa namba ya usajili S.A 23452.

- Dira– Kuhakikisha Ufanisi na uweledi kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala katika Utumishi wa Umma ili kuleta tija iliyokusudiwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

- Dhima– Kukuza viwango na mifumo bora ya taaluma ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala katika Utumishi wa Umma.
Malengo ya Jumuiya
- Kuanzisha jukwaa la kitaifa la Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Tawala katika Utumishi wa Umma ili kupata fursa ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala;
- Kukuza ujuzi na weledi katika eneo la usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Umma miongoni mwa wanachama na wasimamizi wengine;
- Kuhifadhi na kusambaza taarifa za kitaaluma katika kada ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala kwa njia ya tafiti, machapisho, mikutano, ziara za mafunzo, makongamano ya kitaalamu, midahalo na kuweza kujiunga na mitandao ya kitaaluma (professional networks) kitaifa na kimataifa;
- Kuimarisha maadili ya kitaaluma kwenye masuala yanayohusu Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala;
- Kukuza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa kupitia mashirika na taasisi zinazojishughulisha na ukuaji wa usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala;
- Kuimarisha utekelezaji wa mifumo yenye matokeo tarajiwa na shirikishi ya kiutawala ili kufanikisha huduma bora kwa Umma
TAPA-HR MANAGEMENT

Mariamu Emmanuel Mshana
TAPAHR Team Member
I am an expert in Human Resource Management as I have been practicing in the field for more than 15 years.
100%
I sat and pass Professional Examinations for Human Resource Officers from Tanzania Public Service College in 2021.
100%
DIRECTOR OF ADMINSTRATION AND HUMAN RESOURCE MANAGEMENT
Mariam Emmanuel Mshana is the Director